Leo nimetengeneza blog hii ambayo kwa asilimia kubwa itakua inaongelea mainly (sanasana) masuala ya Online Payments (Payments System nyinginezo pia zitaongelewa) ambapo kwa kiswahili nadhani tutasema malipo au kulipia bidhaa na huduma katika mtandao haswa kwa Africa Mashariki.
Blog hii kwanza lugha zote mbili yaani kiingereza na kiswahili zitaruhusiwa kwa sababu hizi:
- Blog hii inalenga zaidi Afrika Mashariki au kimombo East Africa eneo ambalo kiingereza na kiswahili ndizo lugha matata.
- Hapa tunataka yeyote aweze kuchangia (kujadili au kutoa kitu cha kujadiliwa) ili tuweze kupeleka gurudumu hili la Online Payment mbele hapa Africa Mashariki.
- Wanaoweza kiswahili watachangia kiswahili na wanaoweza kiingereza watachangia kiingereza.
- Kuna maneno mengine ya kiteknolojia kidogo yanakua magumu kuyaweka (kuyaexpress) katka kiswahili hivyo mchangiaji wa kiingereza kuruhusiwa kuyatumia maneno hayo moja kwa moja kwa kiingereza ili kuleta maana zaidi.
- Sababu nyingine ni kua pamoja na kwamba Online Payment sio utamaduni wetu lakini nasi tunapenda utamaduni wetu hivyo tuuenzi kwa kufanya kazi kwa kiswahili.
Unaweza changia about cash payments, direct transfer/deposit to bank's account, Money transfer payment, Cheque payment, Online money payment na kadhalika.........(kimombo e.t.c).
Hapa kuchangia kumemaanisha mambo mengi kama;
- Kutoa story au post au link inayoongelea masuala (maendeleo, matatizo, vikwazo) ya payments ziwe online au zile zingine. Masuala hayo yakiwa ni ya East Africa itakua safi na inayopendeza zaidi.
- Kutoa comment na wazo kuhusu masuala ya payment iwe ni kusifia au kuponda au kutoa mchango wa namna ya kupambana na huu uletaji wa online payment
- Kuuliza swali linalokutatiza kuhusu payments haswa online payment online payments. Kama kawa likihusu Afrika mashariki ni poa zaidi.
- Kutupa link ya mradi (project) uwe wako au laa wa mwingine (privacy na terms of use zizingatiwe) ambao unahusu online payments na ukihusu EAC ni bomba au uwe wa mzawa wa EAC.
- meetings, conferences and all other ievents and informations concerning payments and particularly online payments.
WELCOME ALL~*~~~*~~~*~KARIBUNI WOTE
No comments:
Post a Comment